Zitto Kabwe Aibua Mazito Bungeni: Ukiukwaji wa Sheria ya Bajeti, Ufisadi wa Hati Fungani ya Sh1.2 Trilioni
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe jana aliibua mambo mazito bungeni wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Rais –Tamisemi na Utawala Bora, likiwamo la ukiukwaji wa Sheria ya Bajeti kutokana Bunge kupitisha bajeti Sh23.7 trilioni huku Serikali ikija na bajeti ya Sh29 trilioni. Mambo mengine yaliyobainishwa na mbunge huyo ni sakata la ufisadi wa hati fungani ya Sh1.2 trilioni katika Benki ya Standard ya Uingereza na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kushindwa kutoa majibu ya uchunguzi wa miamala kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow kwenda Benki ya Stanbic. Tazama Video Hapa Zitto Akimwaga Cheche: Kuhusu bajeti, Zitto alisema kuna ukiukwaji wa Sheria ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015 katika mchakato wa bajeti ya mwaka 2016/17 kwamba kifungu cha 8 cha sheria hiyo kinaeleza namna ambavyo mfumo wa bajeti ya Serikali unapaswa kuwa. “Vifungu cha 8(1)(b) na 9(1)(a) na 19(1) vinataka ‘mpango na miongozo ya baje...