HII NDIO LIST YA WANAUMEWALIOFAIDI PENZI LA JACKLINE WOLPER
Waliosema ujana maji ya moto hawakukosea kwani una changamoto nyingi hasa pale unapofikia wakati wa kumtafuta mtu sahihi wa kuwa naye maishani yaani mke au mume. Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper anaweza kuthibitisha hilo kwani pengine anaweza kuwa staa mwenye listi ndefu ya wanaume waliomvisha pete za uchumba kisha wakapata walichokitaka na mitini japo haikatishi ndoto zake za kumpata mtu sahihi wa kuwa nae kwenye mahusiano. Katika makala haya tunakuletea listi ya wanaume ambao waliwahi kuwa na Wolper na kumvisha pete za uchumba na wengine kujitambulisha au kumtambulisha kwa wazazi wao,lakini baada ya kufaidi penzi la mrembo huyu things fall apart na kupelekea mrembo huyu kuingia kwenye mahusiano mengine,hali iliyopelekea mashabiki wa muigizaji huyu kuhoji kwanini amekua akiangukia mikonononi mwa matapeli wa mapenzi na wengine wakienda mbali na kudai kuwa pengine mrembo huyu amekua akipenda fedha na sio mapenzi ya kweli kutoka wanaume aliokua nao hapo ...