Siri ya ujambazi Dar bayana
Wadau mbalimbali wakiwamo wananchi, polisi, Jeshi la Wananchi (JWTZ), Wizara ya Mambo ya Ndani wamezungumzia kuongezeka kwa ujambazi katika jiji la Dar es Salaam. Baadhi wamesema matukio hayo ya ujambazi yamesababishwa na udhaifu wa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na wahalifu wanaotumia silaha kupora fedha kwenye mabenki na maduka makubwa. Sababu nyingine zinazotajwa ni majambazi hao kuhukumiwa vifungo vya muda mfupi na kutoka gerezani mapema, hali inayorudisha nyuma juhudi za Serikali kupambana na uhalifu. Kadhalika, umbali wa kituo kimoja cha polisi mpaka kingine, na mara nyingine baadhi kufungwa siku za mwisho wa juma, ni moja ya mambo yanayosababisha kuongezeka kwa uhalifu. Chanzo kingine kilichotajwa kuchochea ongezeko la uhalifu ni kuhujumiwa kwa Jeshi la Polisi na baadhi ya askari wake ambao ama hutoa silaha kwa wahalifu au kushiriki. Maoni ya wananchi Mkazi wa Tandika, Iddi Shomvi alidai jana kuwa majambazi wengi wanaopora fedha kwenye mabenki ni askari wa JWTZ), wali...