Spika Job Ndugai (Mb) Afanya Mabadiliko Mengine ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya mabadiliko mengine ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ili kuzingatia maombi ya baadhi ya Wabunge pamoja na mahitaji mapya yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wa shughuli za Kamati za Bunge. Kwa mujibu wa taarifa yake, mabadiliko hayo yamefanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 116(3) na (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili 2016 ambapo yamehusisha maeneo manne ikiwemo; Kuhamishwa kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati, Kualikwa kwa baadhi ya wajumbe katika Kamati ya Bajeti, Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Haki, Maadili, na Madaraka ya Bunge kuondolewa pamoja na Uteuzi wa wajumbe wapya katika kamati ya Haki, Maadili, na Madaraka ya Bunge. Mabadiliko hayo ya wajumbe kwenye kamati yanaanza mara moja ambapo orodha ya wajumbe waliobadilishwa kamati na nafasi zao ni kama ifuatavyo; Wajumbe wanaohamishwa Kamati ni pamoja na Mhe. Ezekiel Magoyo Maige, (Mb) ambaye alikuwa katika Kamati ya Nishati na Madini na kwa sasa anahamia K...