Unaambiwa P-Square Hawajamaliza Tofauti zao, Walikutana kwa Heshima ya Diamond tu
Wiki iliyopita mashabiki wa kundi hilo walijawa na furaha kubwa baada ya kuwaona pamoja wakishoot video. Kitu ambacho mashabiki wao wa Nigeria hawakijui ni kwamba video hiyo ni ya wimbo walioshirikishwa na Diamond. Wawili hao walienda Afrika Kusini kwa heshima ya Diamond ambaye Paul anamuita ‘The King of East Africa.’ Ukweli ni kwamba matatizo yao yako pale pale na kwa sasa uhusiano wao umebaki kuwa ‘professional’ zaidi na si ule wa kuwa karibu kama ndugu. Hilo unaweza kuligundua hata baada ya wawili hao kumaliza kushoot video hiyo. Kila mmoja alionekana kwenda uwanja wa ndege kivyake na kuna hata uwezekano kila mtu alipanda ndege yake mwenyewe kwenda Jozi na kurudi Lagos. Hakuna picha inayowaonesha wakiwa pamoja airport au ndani ya ndege kama ilivyokuwa zamani. Wakiwa Jozi, hakuna hata picha moja inayowaonesha wakihang out pamoja hotelini, kitu ambacho kwa siku za nyuma kilikuwa ni cha kawaida. Kundi hilo liliingia kwenye mgogoro mk...