Msafara wa Rais Magufuli Kutozidi watu 10.....Balozi Mahega Asema Anategemea Kwenga Ng'ambo hivi Karibuni
Rais John Magufuli anataraji kusafiri tena kwenda nje ya nchi hivi karibuni akiwa na msafara ambao unawezekana usizidi jumla ya watu 10. Ilimchukua Rais Magufuli siku 153 tangu kuapishwa kwake kufanya ziara ya kwanza ya nje ya nchi baada ya kwenda Rwanda kwa mwaliko wa Rais Paul Kagame Jumanne iliyopita. Rais alikwenda Rwanda kwa ajili ya kufungua daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha biashara chenye huduma za pamoja, ambacho ni kiunganishi muhimu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika safari hiyo, katika kile kinachoonekana kuwa ni muendelezo wa hatua yake ya kubana matumizi ya serikali kadri iwezekanavyo, Rais Magufuli alikuwa na msafara usiozidi watu 10. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Mahiga, alisema jana kuwa Rais Magufuli anatarajia kusaifiri tena kwenda nje ya nchi hivi karibuni. Balozi Mahiga alisema katika safari hiyo, msafara wake utaendelea kuhusisha watu wachache wenye umuhimu katika ...