TWAWEZA: 80% YA WATANZANIA WANAAMINI RAIDO..???
Asilimia 91 ya wananchi waliohojiwa wanaitaka Serikali kabla ya kukifungia chombo chochote cha habari ni vema kukifikisha chombo hicho mahakamani ili kutoa fursa ya suala hilo kupitia hatua za kisheria kuliko ilivyo sasa. Mapendekezo hayo yametolewa katika ripoti ya utafiti wa wananchi juu ya haki ya kupata habari iliyofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali ya TWAWEZA ikionyesha kuwa wananchi wengi wanaunga mkono suala la uwazi na uwajibikaji na kuwa upatikanaji wa habari huzuia vitendo vya rushwa. Akiongea wakati wa uwasilishwaji wa ripoti hiyo kwa waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, mshauri mwandamizi wa mawasiliano wa tasisi ya TWAWEZA Risha Chande amesema, Takribani wananchi kati ya wanane na kumi ambao ni sawa na asilimia 78 wanaamini upatikanaji wa habari unapunguza vitendo vya rushwa, huku wanachi kati ya sita na kumi ambao ni sawa na asilimia 68 wamependekeza serikali iwe na mamlaka muhimu ya kuzuia habari zinazotishia usalama wa Taifa. Aidha, ripoti hiy...