Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya  ‘ANAYEWACHEZESHA KAGERA SUGAR NJE YA KAITABA KWA MIEZI 18 SASA NDIYE WA KULAUMIWA WAKISHUKA’

 ‘ANAYEWACHEZESHA KAGERA SUGAR NJE YA KAITABA KWA MIEZI 18 SASA NDIYE WA KULAUMIWA WAKISHUKA’

Picha
Na Baraka Mbolembole Kitendo cha kukubali kufungwa 2-0 na Ndanda SC katika mchezo wao wa 27 ni pigo kubwa ambalo naliona na si ajabu Kagera Sugar ikashuka daraja katika namna isivyotarajiwa na ye yote. Misimu kumi mfululizo yenye kupanda na kushuka kwa timu hiyo ya Misenyi ilijijenga na kuonekana timu yenye uwezo kumaliza nafasi nne hadi 6 za juu katika ligi kuu ya Tanzania. Baada ya timu hiyo kuchukuliwa na kiwanda cha uzalishaji sukari (Kagera Sugar) mwanzoni mwa miaka ya 2000 kutoka kwa wananchi (awali timu hii ilikuwa ikifahamika kama Kagera Stars.) Chini ya mkufunzi marehemu, Slivester Marsh (Mwenyezi Mungu amrehemu) timu hiyo ikafanikiwa kupanda daraja hadi ligi kuu mwaka 2005. Ikashinda taji la michuano iliyopotea ya Tusker Cup mwaka 2007 ikiwa na wachezaji wengi vijana kama Amri Kiemba, Vicent Barnabas na baadhi ya wazoefu kama Yusuph Macho. Omar Changa na Karume Songoro. Kagera ni timu inayowavutia wapenzi wengi wa kandanda nchini kutokana na kuzishinda timu kubwa za Yang...