Serikali ya Tanzania ijibu tuhuma nzito za serikali ya Kenya, rais Magufuli asaidiwe kidiplomasia
Serikali ya Tanzania sasa itoke hadharani kujibu Tuhuma za Serikali ya Kenya na viongozi wa Muungano wa JUBILEE kuwa Rais Magufuli anamdhamini kifedha Kiongozi wa Upinzani Raila Amolo Odinga kusababisha Maandamano, ghasia na hatimaye kuipindua serikali ya Rais Uhuru Kenyatta. Siku Chache Zilizopita Msemaji wa Serikali ya Kenya Erick Kiraithe alisema kuwa tayari kuna taarifa za kijasusi kuwa kuna wanasiasa nchini Kenya wanadhaminiwa na kusaidiwa na Nchi Mbili Jirani maadui wa Kenya kutaka kuvuruga amani na kuiangusha Serikali na kudai kuwa Baraza la Ushauri la Usalama (National Security Advisory Council) lilikutana siku ya Jumatatu kuangalia namna ya kuwashughulikia watu hao Mbunge wa Jimbo la Starehe Mwenye ushawishi ndani ya Serikali ya JUBILEE akiambatana na wabunge wengine alifanya mkutano na waandishi wa Habari Nairobi Hoteli na Kuwataja marais John Magufuli wa Tanzania na Salva Kiir wa Sudan ya Kusini Rais Magufuli akiwa mapumzikoni CHATO msimu wa Sikukuu ya Pasaka alikua Mwe...