Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TANZIA: Mmiliki wa Mabasi ya Ngorika

TANZIA: Mmiliki wa Mabasi ya Ngorika, Stephen Mberesero Afariki Dunia..Agongwa na Gari Akiongea na Simu Segerea

Picha
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Ngorika Bus service, yenye makao yake makuu Kisangara mkoani Kilimanjaro, bw. STEPHEN Mberesero amefariki dunia mjini hapa baada ya kugongwa na gari aina ya Land cruiser wakati akizungumza na simu. Kamanda wa polisi wa MKOA wa Tanga Mihayo msikhera alisema Jana kuwa ajali iyo ilitokea juzi SAA 2;30 usiku katika Barbara kuu ya segera-njiapanda ya himo mjini Korogwe. Alisema Mberesero ambae mabasi yake hufanya safari Kati ya mikoa ya Arusha,tanga,Daresalaam na singida,marehemu alikuwa amesimama pembeni ya kituo cha mafuta cha Lake oil na kugongwa na gari hilo. Mfanyakazi wa kampuni hiyo ,Adam Miraji alisema bosi wake huyo alikwenda Korogwe kuangalia Kiwanja kwajili ya kununua kujenga kituo cha mafuta. Kama unavyojua bosi wetu pamoja na kufanya biashara ya Mabasi,alikuwa anamiliki vituo mbalimbali vya mafuta mkoani Kilimanjaro,Dar es Salaam na Arusha,hivyo alipokuja Tanga alituambia anakwenda Korogwe kuangalia Kiwanja cha kujenga kituo kipya cha mafuta,a...