Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Watu wenye ulemavu wa ngozi Malawi katika hatari ya kuangamizwa kikamilifu

Watu wenye ulemavu wa ngozi Malawi katika hatari ya kuangamizwa kikamilifu

Picha
Watu wenye ulemavu wa ngozi au albino nchini Malawi wanakabiliwa na hatari ya kuangamizwa kikamilifu kutokana na kuongezeka vitendo vya hujuma dhidi yao nchini humo. Hayo yamedokezwa na mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wenye ulemavu wa ngozi, au albino. Ikponwosa Ero ameonya kuwa machungu na vitisho vinavyowakabili albino nchini Malawi vinahatarisha uwepo wao iwapo hatua hazitachukuliwa. Akizungumza baada ya ziara yake rasmi ya kwanza nchini Malawi Bi. Ero amesema albino katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika wanaishi kwa hofu kubwa, hawalali na hata hawawaamini wale wanaopaswa kuwalinda kutokana na familia kuhusika katika baadhi ya matukio ya wao kushambuliwa. Bi. Ero amesema hali ni mbaya zaidi kwa kuwa tangu mwaka 2014 visa 65 vya mashambulizi dhidi ya albino viliripotiwa nchini Malawi vikiwemo visa viwili wakati wa ziara yake. Amesema fikra potofu za matumizi ya viungo vya albino katika ushirikina na kwamba albino hawafariki dunia bali wanatoweka zinahatarisha ...