Trump Achekwa Baada Ya Kushindwa Kulitamka Jina la Nchi yetu Tanzania
Mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani ambaye amekuwa akiongoza kwenye kinyang’anyiro hicho, Donald Trump amejikuta akikosolewa vikali kuhusu upeo wake juu ya sera za nje pale aliposhindwa kulitamka bayana jina la Tanzania. Drump ambaye Jumanne aliyopita alivuna ushindi wa kishindo kwenye majimbo yote manne yaliyopiga kura za mchujo alijikuta akitumbukia kwenye kadhia hiyo wakati akielezea vipaumbele vya Marekani kuelekea mataifa ya kigeni. Alikuwa akigusia juu ya mashambulizi ya mabomu yaliyotokea katika ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na Kenya na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali huku watu kadhaa wakipoteza maisha. Akiwa katika hali ya kujiamini, Trump alisema kuwa iwapo ataingia madarakani moja ya vipaumbele vyake ni kuendelea kutetea masilahi ya Marekani na kudhihirisha hilo aliamua kutolea mfano mashambulizi hayo ya kigaidi. Lakini wakati akilitaja jina la Tanzania, mfanyabiashara huyo alijikuta akigusa hisia za wengi pale alipolitaja jina ...