Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wafanyabiashara Wanaopandisha bei ya sukari kukiona

Wafanyabiashara Wanaopandisha bei ya sukari kukiona

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala amewaonya wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda wanaoficha sukari na kupandisha bei, akisema watachukuliwa hatua za kisheria. Makala alitoa onyo hilo jana alipotembelea Kiwanda cha Sukari cha TPC na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro. “Kamati imejiridhisha kwa kuona uzalishaji na wingi wa sukari iliyopo.Watakaobainika kuagiza sukari nje ya nchi watachukuliwa hatua,” alisema Makala. Aliwataka wafanyabiashara wasifiche sukari kwa kuwa TPC inazalisha ya kutosha kwa mikoa ya Kanda ya Kaskazini. Alisema ni vyema kiwanda hicho kikafanyiwa upanuzi ili kuongeza uzalishaji ambao utasaidia kuongeza mahitaji ya sukari nchini. Alisema uzalishaji mkubwa utaondoa mianya ya uingizwaji wa sukari za magendo. Makala alisema Serikali ilikataza uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ili viwanda vya ndani viuze kwa wingi. Meneja Uhusiano wa TPC, Jafary Ally alisema hawajapandisha bei na kwamba bei ya jumla kwa wasambazaji ni Sh1,750 k...