Wabunge wa CCM Wakataa Bunge Kuonyeshwa LIVE.......Wapinzani Waamua Kujirekodi Kwa Simu Zao
Wabunge wa CCM jana waliibuka kidedea walipowazidi wenzao wa upinzani kwa kura za sauti “Siyooooo” kuikataa hoja ya kutaka matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja ‘live’ na televisheni. Hiyo ilitokea jana wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya Ofisi ya Rais (Tamisemi na Utumishi na Utawala Bora) na kuzua mvutano mkali uliosababisha bajeti hiyo ipitishwe kwa utaratibu wa wabunge kutohoji kitu chochote (guillotine). Wakati hoja yao hiyo ikipingwa kila kona, tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, wabunge hao wa upinzani sasa wamebuni mbinu mpya ya kujirekodi wenyewe wakati wakichangia mijadala mbalimbali bungeni na kurusha sauti zao kwenye mitandao ya kijamii na kupeleka sauti hizo kwenye redio zilizopo katika maeneo ya majimbo yao. Mbunge wa Malindi (CUF), Ally Salehe ndiye aliyeibua hoja hiyo akitaka kushika mshahara wa waziri kwa maelezo kuwa kuzuia Bunge kurushwa ‘live’ ni kinyume na utawala bora na haki ya kupata habari. Hoj...