VITAMINI C NA NGOZI YENYE AFYA
Vitamini C(ascorbic acid) ni miongoni mwa kundi la vitamini zinazochanganyika na maji(B na C). Uwezo wa kuondoa sumu (antoxidants) wa vitamini C na usaidizi wake katika kutengeneza kollageni, huifanya vitamini hii kuwa muhimu kwa afya ya ngozi. Tafiti zinaonyesha kuwa matumizi ya vyakula vyenye vitamini hii, ni yenye faida kwa seli za ngozi, na tafiti hizi pia zimeonyesha kuwa vitamini C husaidia kuzuia madhara ya mionzi hatari kutokana na miale ya jua (U.V radiation) na pia kusaidia kupona kwa haraka ngozi iliyoathirika na mionzi hiyo hata pia maambukizi ya vijimelea. Matumizi makubwa ya vyakula vyenye Vitamini C yamekuwa yakihusishwa na kupungua kwa hatari ya kuwa na ngozi iliyo kavu na iliyokunjamana, na hii inadhihirisha kuwa Vitamini C huzuia upotevu wa maji kutoka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuwa nyororo. Ni muhimu na kujitahidi mlo wako kuwa na vitamini C ya kutosha kutokana na umuhimu wake kwa ngozi yako. Uwezo wa vitamini C kuondoa sumu pamoja na kusaidia ut...