Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Bunge kuanza kutumia mfumo mpya wa kurusha matangazo kwa njia ya Satellite

Bunge kuanza kutumia mfumo mpya wa kurusha matangazo kwa njia ya Satellite

Picha
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanya mabadiliko ya kurusha matangazo yake ambayo yanaviwezesha vyombo vya habari (redio na tv) kupata matangazo hayo moja kwa moja bila kufunga mitambo yao katika eneo la bunge. Katika taarifa ambayo imetolewa na kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha bungeni imeeleza kuwa mfumo huo utakuwa ukirusha mtangazo kupitia satellite ambapo vituo vya redio na runinga vitakuwa vikitumia satellite kupokea matangazo hayo na kuyarusha katika vituo vyao. Taarifa hiyo imeeleza kuwa redio na vituo vya runinga vitakuwa vikiyapata matangazo kupitia satellite Intelsat 17, nyuzi 66 upande wa Mashariki. SATELLITE: Intelsat 17 @ 66 East FREQUENCY: 11024.2500MHZ SYMBOLRATE: 3071.8 Mbps POLARIZATION: Horizontal FEC: 1/2 MODULATION: 4PHASE-QPSK AUDIO: CH. 1…noneI, CH.2…none, CH.3…TV Audio na CH. 4…Radio Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa mfumo huo ndiyo unaotumika na mabunge mengi duniani na kutumika kwa mfumo huo hakuwazuii ...