JOE HART AINYIMA MADRID USHINDI
Joe Hart ameendelea kuipa matumaini Manchester City ya kufika hatua ya fainali ya Champions League kwa mara ya kwanza baada ya kuokoa michomo miwili ya hatari wakati wa mchezo wa kwanza wa nusu fainali dhidi ya Real Madrid uliomalizika kwa sare ya bila kufungana. Ikicheza bila striker wake nyota Cristiano Ronaldo ambaye yuko nje kwasababu ya majeruhi, Real Madrid walifanya mashabulizi machache yenye uhai langoni mwa City hadi dakika za mchezo huo zinamalizika. Dakika ya 20, Jese alipiga mpira kichwa ambao uligonga ‘mtambaa panya’ wa goli ya City kabla ya Hart kuokoa michomo ya Pepe na Casemiro iliyotokana na mipira kona. Hart alionesha uwezo wa hali ya juu kuokoa kwa mguu mpira wa kichwa uliopigwa na Casemiro lakini baadaye alimnyima Pepe goli akiwa umbali wa mita tano kutoka lilipo goli, Hart amekuwa sababu ya City kusafiri kwenda Hispania wiki ijayo huku ikiwa na clean sheet. Nafasi ya City kupata bao ilikuwa ni pale ambapo dakika za lala salama ambapo Kelvin de Bruy...