Mjane Wa Baba Wa Taifa, Mama Maria Nyerere Atembelea Daraja La Nyerere Kigamboni Leo
Mke wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Maria Nyerere ametembelea Daraja la Nyerere linalounganisha eneo la Kigambaoni na Kurasini Jijini Dar es salaam na kuipongeza serikali na wananchi wote wa Tanzania kwa kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo kubwa na la kisasa kwa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati. Mama Maria Nyerere aliyeongozana na Mwanae Mheshimiwa Makongolo Nyerere amesema kukamilika kwa daraja hilo ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 254.12 kumekamilisha mpango wa miaka mingi ulioanzishwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa na nia ya kujenga daraja katika eneo hilo la mkondo wa bahari lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti haikuwezekana. Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuamua Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere kwa heshimu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na amebainisha kuwa uamuzi huo utaviwezesha vizazi vijavyo ...