Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya NAY WA MITEGO NA NIVA WAVUANA NGUO HADHARANI

NAY WA MITEGO NA NIVA WAVUANA NGUO HADHARANI

Picha
Baada ya lile drama kati ya star wa Bongo movie, Niva Supermariyo, na Nay wa Mitego kushika moto kutokana na wimbo wa 'Shika adabu yako' ya Nay na Niva kuamua kumjibu kupitia filamu ambayo aliipa jina la 'Maisha ya mtoto wa Manzese' Sasa mastaa hao wameamua 'kuvuana nguo' hadharani kwa kila mmoja kuamua kumponda mwenzake. Wakizungumza na Enewz kwa wakati tofauti tofauti ili mastar hao waweke bayana tofauti zao lakini waliamua kutoleana uvivu kwa kupigana madongo ya live bila kukwepeshana. Alipoulizwa Niva kwanini aliamua kuingia kambi ili kuandaa filamu tu itakayo mponda Nay? Niva alisema “Nay ni kama babaji kwahiyo hawezi shindana na mimi haniwezi kama yeye alizoea kuwaonea wanyonge mimi sasa haniwezi ,kimaisha kwanza hajanifikia na mtu mwenye akili huwezi kujianika sana vitu vyako vya ndani kama yeye anajiona star, kwanini anakimbiwa na wanawake”. Enewz haikuishia kufanya mahojiano na Niva, Ilimlazimu kumtafuta Rapper Nay Wamitego kujua nini mtazamo wake...