Makumi ya maelfu ya watoto nchini Somalia wakabiliwa na hatari ya kifo
Mkuu wa Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Pembe ya Afrika amesema watoto wapatao 60,000 nchini Somalia wanakabiliwa na hatari ya kifo kutokana na uhaba wa misaada ya kibinadamu.Akizungumzia suala hilo hivi karibuni, Peter de Clercq, Mkuu wa Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa kutokuwepo uthabiti wa kisiasa na kukumbwa nchi hiyo na ukame wa mara kwa mara na hata mara nyingine mafuriko ni mambo ambayo yamepelekea watu wapatao milioni 5, yaani karibu nusu ya raia wa nchi hiyo kuhitajia misaada ya dharura ya kibinadamu. Ukame na mafuiriko yanayosababishwa na mabadiliko yasiyotabirika ya hali ya hewa yanayojulikana kwa jina la El Nino yamezidisha idadi ya watu wanaokumbwa na baa la njaa barani Afrika na hasa katika nchi za Kaskazini mwa Sudan na eneo lililojitangazia utawala wa ndani la Puntland. Hii ni katika hali ambayo ili kukabiliana na mgogoro huo wa kibinadamu Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuchangishwa dola milioni 885...