Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mhe. Truong Tan Sang Awasili Tanzania

Rais Wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Awasili Tanzania

Picha
RAIS wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Truong Tan Sang, amewasili  nchini  jana  saa  mbili  usiku tayari kwa  kuanza ziara ya siku tatu nchini, ambapo pamoja na masuala mengine, atasaini mkataba wa masuala ya Kodi na mwenyeji wake Rais John Magufuli. Mkataba huo unalenga kuchochea biashara kati ya Vietnam na Tanzania kwa kuwa utatoa fursa kwa wafanyabiashara wa pande zote kutotozwa kodi mara mbili katika biashara na uwekezaji watakaoufanya. Rais huyo anatarajiwa kupigiwa mizinga 21 leo, ikiwa ni pamoja na kukagua gwaride rasmi, ambapo baadaye atatambulishwa kwa viogozi mbalimbali wa Serikali, kabla ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa Dar es Salaam kuhusu ujio wa Rais huyo wa Vietnam, baada ya viongozi hao kutia saini mkataba huo, mgeni huyo na ujumbe wake atakwenda kwenye ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyopo katika Mtaa wa Lumumba jijini humo kukutana na Mwenyekiti wa chama hicho, ambaye ni Rais ms...