Burundi yakaribisha kuteuliwa mpatanishi mpya mgogoro wa nchi hiyo
Burundi imeunga mkono kuteuliwa mpatanishi mpya kwa ajili ya kujaribu kutatua mgogoro wa nchi hiyo. Chama tawala cha CNDD-FDD jana Alkhamisi kilisema kuwa kuteuliwa Benjamin William Mkapa, rais wa zamani wa Tanzani akuwa mpatanishi mpya wa nchi hiyo ni hatua nzuri katika kuharakisha juhudi za kutatua mgogoro wa nchi hiyo.Pascal Nyabenda, mwenyekiti wa chama hicho amesema Mkapa ana wakati mwingi wa kuzungumza na mirengo pamoja na wananchi wa Burundi ili kuandaa mazingira ya kufikiwa matokeo mazuri ya kurejeshwa amani na uthabiti nchini Burundi. Kiongozi huyo wa Burundi amesema kuwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda ataendelea kusalia katika nafasi yake ya kusaidia kuboresha mazingira ya mazungumzo ya Burundi lakini kwamba yeye peke yake hawezi kusimamia mazungumzo hayo. Katika kikao chao cha hivi karibuni viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walimteua Benjamin Mkapa kuwa mwenyekiti wa kundi la upatanishi wa mgogoro wa Burundi. Awali Museveni alikuwa ameteuliwa kuwa mpatanishi wa mgogor...