UKAWA Wawakaanga Ridhwan Kikwete na Mama Salma
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imewakaanga wanaotajwa kumiliki Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) bila kufuata utaratibu, anaandika Pendo Omary. Hatua hiyo imekuja baada ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inayoongozwa Ukawa kuzuia Sh. 5 bilioni, fedha mali ya Kampuni ya Simon Group Limited. Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na Ridhwan Kikwete, mtoto wa rais huyo na Prof. Juma Kapuya, aliyekuwa Mbunge wa Urambo Magharibi wanatajwa kuwa miongoni mwa wana hisa kwenye shirika hilo. Simon Group Limited ililipa fedha hizo kwa halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya malipo ya ununuzi wa hisa za UDA. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo amesema halmashauri haikuuza UDA licha ya Simon Group Limited kudai kununua. Kwenye mkutano huo ambao pia uliohudhuriwa naIsaya Mwita Charles, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Kubenea amesema, mkutano uliokabidha UDA kwa Simon...