Pigania Ndoa Yako Si Michepuko ya Mumeo..
NIMEIKUTA MAHALI NIKAONA NI VIZURI KU-SHARE Kuna dada mmoja nikikuwa namfahamu miaka mingi sana. Kama miama 15. Kipindi hicho tukiwa ni wasichana wa miaka 25. Dada huyo ghafla akawa na mahusiano na mume wa dada yangu. Nilimchukia sana. Dada yangu alimchukia sana. Wote tulimchukia. Alikuwa mlevi. Malaya na anayependa kuvaa uchi. Hakuwa anajijali hata kidogo. Mimi na Dada yangu tulikuwa tunatamani hata afe ama akatike miguu kwa namna alivyokuwa malaya na mshenzi. Miaka ikapita. Kila ninapokutana na dada yangu haishi kunikumbusha Dativa. Kila siku tulikuwa tunamuongelea. Na kutamani tusikie hata kuna msiba kwao na amefariki dunia. Baada ya miaka mitano kupita. Mimi nikiwa nimeahamaliza masomo yangu. Na sasa na niko kazini nafanya kazi yangu nzuri tu. Kijana mmoja akaniambia ananipenda na anataka kunioa. Miaka yote hiyo sikuwa na mahusiano kwani nilijua na mimi kina Dativa wataharibu ndoa yangu. So sikupenda ndoa kabisa. Hivyo kijana huyo nikamkataa. Ni kijana kama wa 10 hivi kumkat...