Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CCM Yakanusha Mwenyekiti wake Jakaya Kikwete 'Kugoma' Kukabidhi Uenyekiti kwa Rais Magufuli

CCM Yakanusha Mwenyekiti wake Jakaya Kikwete 'Kugoma' Kukabidhi Uenyekiti kwa Rais Magufuli

Picha
Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa  Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya Chama Cha Mapinduzi. Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti. Habari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dkt. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo.  Kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa kusiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu ya kukamilisha maandalizi ya agenda hizo. Alisisitiza agenda iwe moja tu. Dhamira ya kufanyika Mkutano Mkuu maalum mwezi Juni, 2016 iko pale pale. Kilichoelezwa kwenye kikao ni kutaka kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo.  Taratibu zikikamilika tarehe itapangwa. Mipango ya kutafuta pesa inaendelea na ikikamilika tarehe itatangazwa. Tunawataka wana-C...