Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya HATIMAYE SIWEMA WA NAY WA MITEGO ATOKA GEREZANI

HATIMAYE SIWEMA WA NAY WA MITEGO ATOKA GEREZANI

Picha
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mzazi mwenzake,  Siwema Edson Mzazi mwenzake Nay wa Mitego, Siwema Edson. Na Gladness Mallya,  RISASI MCHANGANYIKO HABARI njema! Mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson aliyehukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la kutishia kwa njia ya mtandao, hatimaye ametoka jela. Akipiga stori na  Risasi Mchanganyiko , Nay wa Mitego alisema katika harakati za kushughulikia ili mzazi mwenzake huyo atoke alifanikiwa kupata mawakili wawili ambao mpaka Jumamosi iliyopita walifanikisha zoezi la Siwema kutoka na sasa atatumikia kifungo cha nje. Nay wa Mitego alisema alilazimika kupambana kwa nguvu zote si kwa sababu anataka kuwa naye isipokuwa kama mzazi hakujisikia vizuri kuona mama wa mwanaye yuko jela wakati yeye anao uwezo wa kufanya kitu kwa ajili ya kumsaidia. “Kulikuwa kuna njia mbili za kufanya, kukata rufaa au kubadilishiwa kifungo, mawakili wangu waliniambia n...