Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya OSCAR JOSHUA: HATUWEZI KUINGIA KATIKA USHAWISHI ‘MBAYA’ KUHUSU ESPERANCA

OSCAR JOSHUA: HATUWEZI KUINGIA KATIKA USHAWISHI ‘MBAYA’ KUHUSU ESPERANCA, HIKI NI KIKOSI KIKALI ZAIDI YANGA

Picha
Baraka Mbolembole Wakati Yanga SC ikiangalia jinsi gani ya kuifunga Esperanca ya Angola na kuitoa katika ‘play off’ ya michuano ya Shirikisho Afrika siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mlinzi wa kushoto wa timu hiyo, Oscar Joshua anasema kwamba hawatashawishika kwa namna yoyote ile kuamini mtazamo wa baadhi ya watu kwamba Waangola hao si timu kali. “Hii si nafasi ya wazi kwetu, na hatufikirii kabisa kwamba wapinzani wetu wajao katika michuano ya CAF ni timu rahisi. Hatuwazii hivyo, tunavyojua sisi (Yanga) Esperanca ni timu ngumu na lazima tujiandae kushinda na wala hatupo tayari kupokea mawazo kuwa hiyo ni timu rahisi. Hatushawishiki kwa hilo hata kidogo”, anasema Oscar wakati nilipofanya naye mahojiano marefu akiwa mkoani Shinyanga ambako aliisaidia timu yake kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji wao Stand United katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara siku ya Jumanne. Yanga itacheza mchezo wa kwanza nyumbani, na hawatapaswa kwa namna y...