Sheria 8 Za Kukusaidia Kufanya Biashara Yako Kwa Mafanikio Makubwa
Kila kitu kilichopo dunia kinaongozwa na sheria zake. Sheria hizo zinapotumika ipasavyo mara nyingi sana huleta mafanikio makubwa. Na inapotokea sheria hizo zikavunjwa hakuna mafanikio yanayokuwepo zaidi ya kushindwa kwa wale wote waliovunja sheria hizo. Haijalishi upo katika eneo gani sheria ni muhimu sana kuzingitiwa. Iwe katika afya, elimu, mchezo wa mpira wa miguu, au biashara sheria huwa zipo na zinafanya kazi. Sheria hizi ndizo zinazotupa mwongozo bila kujali uwe unazijua au huzijui lakini zipo, ukikosea unahukumiwa. Katika makala hii tutajifunza sheria zitakazo kusaidia kufanya biashara yako kwa ushindi. Bila shaka umekuwa ukiona wengi wakifanya biashara zao kwa mazoea sana. Kutokana na mazoea hayo hupelekea biashara nyingi kugeuka kuwa kama ‘miradi bubu’ ambayo haina faida yoyote. Sitaki hilo lizidi kukutokea sana la kufanya biashara ambayo haikupi faida kubwa unayoifikiri kwa muda mrefu. Inabidi ukubali umekosea na kaa chini ujifunze sheria za msingi kabisa amba...