Madaktari Wataka Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) Itumbuliwe
Waganga wafawidhi wa Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, wamesema Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) ni “jipu” linalohitaji kutumbuliwa kutokana na kuwa na mfumo usioridhisha wa utoaji huduma za dawa. Wakizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, madaktari hao walisema MSD inahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa ya utendaji kazi wake, kama siyo kutumbuliwa kutokana na kuwafanya wafanye kazi katika mazingira magumu na yasiyo na dawa. Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Azizi Msuya alisema changamoto iliyopo ni upatikanaji wa dawa na mara nyingi wanachoomba MSD sicho wanachopata na kinawaletea uhasama na chuki kwa wagonjwa. “Wao wananunua palepale na sisi tungeruhusiwa tungenunua. Maduka kama Salama, kopo moja la dawa aina ya paracetamol ni Sh7,000, lakini tukinunua kwao inakuwa Sh15,000 la sivyo turuhusiwe kununua wenyewe kuliko kusubiri dawa mwezi mzima,” alisema Msuya. Alisema unaweza kuomba dawa aina nyingi zikiwamo za kuponya maisha haraka k...