Mbunge Nusura… Akamatwe na ‘unga’ Dar
Kamanda wa Kitengo cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya, ACP Mihayo Msikhela Na Makongoro Oging’, UWAZI Dar es Salaam: Jeshi la Polisi Kitengo cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya, wiki iliyopita nusura limnase mbunge mmoja kutoka jimbo moja lililopo katika moja ya mikoa ya pwani (jina linahifadhiwa) baada ya kumuwekea mtego kutokana na madai kwamba alikuwa akisafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ kutoka kwenye ufukwe mmoja wilayani Bagamoyo kuelekea jijini Dar. Taarifa zilizopatikana kutoka kwa vyanzo vyetu ndani ya jeshi hilo zinadai kuwa, msamaria mwema mmoja alivujisha siri kwa jeshi hilo kwamba, mbunge huyo amebeba unga kwenye gari lake dogo akielekea Dar ambapo bila kupoteza muda, polisi walimuwekea mtego kabambe kwenye njia ambazo alitarajiwa kupita ambapo hata hivyo, aliukwepa baada ya kubadilisha njia. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, mbunge huyo alikuwa akipita usiku wa saa mbili na mzigo huo lakini inadaiwa kuwa alishtukia kwamba amewekewa m...