Wasomi Wahoji Ububu wa UKAWA Bungeni....
UAMUZI wa Kambi ya Upinzani bungeni kuingia katika vikao vya Bunge na kugeuka bubu wakati wa mjadala wa Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, umechukuliwa kwa hadhari kuwa unaweza kusababisha kambi hiyo ionekane inalinda posho bungeni. Hadhari hiyo imetolewa na wasomi na viongozi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili jana, walipokuwa wakitoa maoni kuhusu uamuzi wa kambi hiyo kususa hotuba hiyo. Dk Bana Mhadhiri wa fani ya siasa na utawala katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, ndiye aliyesema kuwa kama uamuzi huo wa kuwa bubu bungeni hautabadilishwa, kambi hiyo itaonekana inalinda posho na kwamba haipo kwa ajili ya kutetea wananchi. “Kazi yao ni kuwakilisha wananchi na makundi yote bungeni, sasa kitendo cha kuota ububu na kushindwa kueleza kero za wananchi, ni kutotendea haki wananchi maana ni vema wakae bungeni na kutoa hoja zao la sivyo, itafika wakati watatuomba radhi wananchi,” alisisitiza. Akizungumzia hoja ya kwanza ya Mw...