Rais Magufuli Amteua Dk Asha-Rose Migiro Kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza. Dkt. Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani. Dkt. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma. Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dodoma 04 Mei, 2016 ------------------------------- Mapito ya Dk. Migiro Dk. Migiro alizaliwa tarehe 9 Julai 1956 katika Wilaya ya Songea, Ruvuma. Alisoma Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, Dar es Salaam mwaka 1963 hadi mwaka 1966. Dk. Migiro alihamia Shule ya Msingi Korogwe, Tanga ambapo aliendela na elimu ya msingi mwaka 1967–1969. Baadaye akajiunga kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Weruweru, Kilimanjaro mwaka 1970 hadi 1973 na Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari Korogwe mwaka 1974 -1975. Dk. Migiro alikuwa mmoja ...