MADAI YA DIAMOND PLATINUMS KUWA NA DHARAU HAYA HAPA
Madai! Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenyooshewa kidole na baadhi ya watu wake wa karibu tangu kitambo wakidai kuwa, toka kuukwaa umaarufu kupitia sanaa hiyo na kusemekana akaunti yake benki inasoma shilingi bilioni 8, amekuwa na dharau wakiitaja ni kwa asilimia mia moja, Amani lina kila kitu. Kwa mujibu wa watu hao, wakiwemo waliyosoma naye shule ya sekondari, Diamond wa sasa si yule wa zamani kwa vile ana fedha nyingi na ana jina kubwa huku pia akijulikana kimataifa. DIAMOND (1)SIKIA HII “Jamani nataka kuwaambia jambo moja kuhusu dogo Diamond. Huyu jamaa tangu amepata jina na tangu amekuwa na akiba benki sijui bilioni nane, hashikiki. Maana nilisoma kwenye mtandao, basi anajisikia sana. “Imefika mahali dogo nampigia simu hapokei wala nikimtumia meseji hajibu. Hii mimi naona ni dharau kwa asilimia mia moja. Diamond amesahau nyuma alikotoka. Mimi sasa ni kama shabiki wake, kwa hiyo asisahau kwamba ndiyo tumemfikisha alipo....