Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Rais Magufuli Atishia Kuwatumbua JIPU Mawaziri Wawili......Wenzao Wabaki Vinywa Wazi Kikaoni

Rais Magufuli Atishia Kuwatumbua JIPU Mawaziri Wawili......Wenzao Wabaki Vinywa Wazi Kikaoni

Picha
Operesheni ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri wawili ambao  pia walikuwa  manaibu  mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne. Taarifa kutoka katika chanzo cha kuaminiwa zimeeleza kuwa Rais Magufuli alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Mawaziri hao na kuwafokea mbele ya mawaziri wenzao  kwa kuwataja majina katika kikao maalum cha mawaziri kilichofanyika hivi karibuni. "Ni mazingira ambayo mawaziri hawakuyazoea kwamba Rais anawaambia moja kwa moja kwa majina, anafoka akisema anaweza kuwafukuza wakati wowote..... "Mawaziri wamezoea mara kwa mara wanapofanya kosa au uzembe wanaonywa kwa staili tofauti, ni kama ya kistaarabu hivi. Sasa huyu bwana mkubwa hana mchezo, aliwataja kabisa, tena mbele ya wenzao ambao walibaki vinywa wazi. “Wewe (anataja jina la Waziri) na mwenzako (anamtaja jina pia) nitawatumbua,”  Chanzo cha gazeti la Rais Mwema kinamkariri Rais Magufuli. Mawaziri hao ambao ni wabunge wa kuchaguliwa maj...