Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mizengo Pinda ( Mtoto wa Mkulima ) Aishi Maisha ya Kikulima

Mizengo Pinda ( Mtoto wa Mkulima ) Aishi Maisha ya Kikulima

Picha
WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, maarufu kama Mtoto wa Mkulima, ameamua kuishi maisha tofauti kabisa na watangulizi wake kwa kukwepa kukaa jijini Dar es Salaam na kwenda kijijini kwake baada ya kustaafu. Pinda aliwahi kukiri kwamba hana nyumba jijini Dar es Salaam zaidi ya kibanda kidogo kilichoko Pugu, ambacho hakina hadhi ya kuishi mtu. Mtoto huyo wa mkulima amejichimbia katika kijiji cha Makanyagio, Mpanda mkoani Katavi, akiendesha shughuli za kilimo na ufugaji, tofauti kabisa na watangulizi wake ambao baada ya kustaafu waliendelea kuishi jijini Dar es Salaam. Tangu awamu ya nne ilipoondoka Ikulu Novemba 5, mwaka jana, Pinda hajawahi kufanya safari yoyote nje  ya nchi na wala kujihusisha na shughuli za kitaifa na kijamii kama walivyokuwa watangulizi wake. Aidha, Mizengo Pinda amepotea kwenye vyombo vya habari kama watangulizi wake. Mtoto wa Mkulima ni jina ambalo alijipachika mwenyewe baada ya kuteuliwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2008 kuwa Waziri Mkuu. Pinda...