MSANII TANZANITE AMUOMBA MSAMAHA DIAMOND PLATNUMZ
Tanzania amemuomba Diamond Platnumz msamaha kwakosa la kurudia wimbo wake wa Mbaga na kudai kuwa Diamond alimroga. Dully skyes ambaye ameanza kumsimamia msanii huyo amesema bila ya kumuomba msamaha Diamond ataendelea kuwa na laana ya kimuziki. Tanzanite ambaye kwasasa amebadilisha jina na sasa anajiita Tanzamagic amemuomba Diamond msamaha pamoja na uongozi wa WCB na mashabiki zake wote. Miaka zaidi ya mitano iliyopita diamond platnumz ali release wimbo unaitwa mbagala, haukupita muda akaibuka msanii anaitwa tanzanite na kutoa ngoma inaita Uchawi na wanga ambayo beat yake ilikua ni ile ile ya mbagala. Drama zilitokea nyingi tanzanite akadai kuwa diamond alimwibia beat na ku copy melody, baada akaja kusema kuwa diamond amempiga juju, sasa miaka imepita diamond platnumz amezidi kuwa mkubwa huku akiwa na zaidi ya tuzo za ndani na za kimataifa zaidi ya 35 kwenye kabati lake, sasa tanzanite ameibuka tena, tyme akiwa yuko kwenye mikono ya legendary dully sykes under studio 4...