Ofisa wa TRA na Mfanyakazi Mmoja wa Yono Auction Mart Wafikishwa Mahakamani Kwa Rushwa
Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Amani Mkwizu na mfanyakazi wa kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, Edward Magobela wamepandishwa kortini jana wakikabiliwa na mashtaka matatu ya rushwa. Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakidaiwa kuomba rushwa ya Sh50 milioni na nyingine ya Sh5 milioni na kupokea Sh3 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Commercial Sales and Services Tanzania Limited, Glenn Clarke. Akiwasomea mashtaka yao, Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Denis Lekayo alidai washtakiwa hao waliomba na kupokea kiasi hicho cha fedha ili kumwezesha mkurugenzi huyo kupunguziwa kodi aliyokuwa anadaiwa kutoka Sh375 milioni hadi Sh100 milion. Hata hivyo, washtakiwa hao walikana mashtaka na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Hakimu Huruma Shaidi anayesikiliza kesi hiyo, aliwaeleza washtakiwa hao k...