Mahakama ya Rufani Yatengua Hukumu ya Mahakama Kuuu Dhidi ya Bosi wa Zamani wa TRA na Wenzake......Yaamuru Jalada Lirudi Mahakama Kuu Kwa Ajili ya Kusikilizwa
Mahakama ya Rufani Tanzania, imeamuru jalada la kesi inayomkabili Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kurudishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa rufani ya Jamhuri. Pia, imeagiza jalada hilo lipangiwe kusikilizwa kwa jaji mwingine dhidi ya rufaa ya kupinga kuondolewa shtaka la utakatishaji fedha katika kesi ya kujipatia Dola za Marekani milioni 6. Hukumu hiyo ilisomwa jana na Msajili wa Mahakakama ya Rufani, Zahra Maruma baada ya kusikilizwa na jopo la majaji watatu, likiongozwa na Mwenyekiti Salum Masati akisaidiana na Kipenka Musa na Augustine Mwarija. Msajili Maruma alisema mahakama hiyo imeona kwamba Jaji Mfawidhi Moses Mzuna alikosea kukubali pingamizi la utetezi na kutupilia mbali kusikiliza rufani ya kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wa kuliondoa shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya Kitilya na wenzake. “Mahakama hii imebatilisha uamuzi uliotolewa na Jaji Mzuna na kwamba i...