Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kilio cha wafanyakazi waliomzuia Majaliwa chamfikia waziri

Kilio cha wafanyakazi waliomzuia Majaliwa chamfikia waziri

Picha
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama, amesikiliza kilio cha wafanyakazi wa Kampuni ya Tarmal ambayo ni Wakala wa Kampuni ya PSI. Jenista alikwenda jana kusikiliza kilio cha wafanyakazi hao baada ya juzi kumfikishia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, baada ya kuzuia msafara wake uliokuwa ukitoka katika hafla ya kupokea vifaa tiba vyenye thamani ya Sh bilioni 10 vilivyotolewa na umoja wa kampuni zinazozalisha vinywaji laini kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Wafanyakazi hao waliopo katika Ghala la PSI lililopo Mabibo jijini Dar es Salaam, waliuzuia msafara wa Waziri Mkuu na kumwambia baadhi ya kero wanazokumbana nazo wawapo kazini. Baada ya Jenista kufika katika ofisi za kampuni hiyo, aliwapa muda wafanyakazi kutoa malalamiko yao na kwa kupokezana walisema kilio chao kikubwa ni suala la mishahara midogo pamoja na mikataba. Pia walisema jambo jingine ni makato yao ya mishahara kutopelekwa katika Mfuko wa Pensheni wa PPF. ...