HUWEZI AMINI YATIMA MASKINI AKATAA KUASILIWA NA KIM KARDASHIAN!
Mtoto aliyekuwa akiishi katika mazingira ya umasikini katika Nyumba ya kulea Watoto yatima nchini Thailand amefanya uamuzi wa kushangaza alipokataa ombi la Nyota maarufu duniani Kim Kardashian kumuasili kuwa sehemu ya familia yake. Taarifa zinasema binti huyo alifurahi sana aliposikia milionea huyo anataka kumuasili, lakini alisisitiza kuwa anataka kusoma nchini Thailand akimtaka Kim kuisaidia nchi yake na watoto wenzake wanaoishi pamoja katika nyumba ya watoto yatima.Kim alivutiwa na binti huyu aitwae Pink mwenye umri wa miaka 13, alipotembelea nyumba ya watoto yatima katika Jimbo la Phang Nga,eneo ambalo zaidi ya watu 4,000 walipoteza maisha kutokana na Tsunami mwaka 2004. Pink alipelekwa na mama yake katika nyumba ya kulelea watoto kwa kuwa hakuweza kumlea mtoto huyo na kugharamia elimu yake. Binti huyu anasema yeye na Watoto wenzake walipokutana na Kim Kardashianhawakumfahamu yeye ni nani. Pink ambaye jina lake halisi ni Laddawan Tong-Keaw, alifurahi kukutana na Nyota huyo, a...