Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAULID MTULIA : Nitawaondoa Panya Road

MAULID MTULIA : Nitawaondoa Panya Road, wauza unga

Picha
Dar es Salaam. “Wilaya yetu ya Kinondoni inakabiliwa na janga la dawa za kulevya na vikundi vya vijana waporaji maarufu Panya Road. Inabidi tufanye jitihada kuwaokoa na hii ni moja kati ya vipaumbele vyangu.” Ndivyo Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF) alivyoanza kuzungumza na gazeti hili kuhusu maisha yake, familia na majukumu aliyo nayo katika jamii. Mtulia alishinda jimbo hilo kwa kupata kura 70,337 na kumuangusha mbunge wa zamani, Idd Azzan aliyeshika nafasi ya pili kwa kura 65,964. Umaarufu wa mbunge huyo uliongezeka zaidi wakati wa sakata la bomoabomoa lililowakumba wakazi wa Mkwajuni, baada ya kuamua kufungua kesi ya kupinga nyumba za wananchi wake kubomolewa bila kuwapo kwa njia mbadala ikiwamo kupatiwa makazi mengine yenye usalama zaidi. Anasema mkakati wake ni kuhakikisha wanajiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa kwenye halmashauri kupitia fedha zilizotengwa kwa ajili ya vijana. Anatarajia kufanya kikao ...