Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TAKURURU Washtuka Sasa Yaanza Kuchunguza Mabilioni ya Kikwete

TAKURURU Washtuka Sasa Yaanza Kuchunguza Mabilioni ya Kikwete

Picha
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza kuchunguza fedha za uwezeshaji maarufu kama ‘Mabilioni ya JK’ ambazo hazikurejeshwa na wakopaji nchi nzima.  Msemaji wa Takukuru, Tunu Mleli alisema jana kuwa taasisi hiyo imechukua jukumu hilo kwa sababu moja ya majukumu yake ni kuchunguza masuala ya rushwa na kutoa rai kwa mtu mwenye ushahidi au taarifa kuhusu suala hilo kuzitoa kwa taasisi hiyo.  “Takukuru ipo wazi kuzipokea taarifa hizo ili zitusaidie kwenye uchunguzi,” alisema Tunu. Kati ya Sh50 bilioni zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, ni Sh43 bilioni tu zilizorejeshwa, huku Sh7 bilioni zikidaiwa kutafunwa.  Fedha hizo zilitolewa na Kikwete kwa ajili ya kuwawezesha kimitaji, wajasiriamali nchi nzima, mikopo ambayo ilipitia benki za CRDB, NMB, Community Bank na Benki ya Posta Tanzania.  Fedha hizo kutoka Mfuko wa Rais, zilikuwa zikikopeshwa kwa riba ya asilimia 10, ambapo a...