Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (Ovarian Cyst) (PLIZ SHARE)

UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE (Ovarian Cyst) (PLIZ SHARE)

Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary) hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama 'Ovarian Cyst'. Uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa umri wowote ule na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. Lakini kwanza hebu tuelezee juu ya mayai ya mwanamke. Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto kwake. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (Uterus). Mayai haya ya mwanamke huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama 'Ovum' na mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (Ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni. Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, masaa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo aina ya 'Luteinizing Hormone' kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa katika kila 'Ovari' na hii...