Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Marekani yaipatia Tanzania dola milioni 800 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo

Marekani yaipatia Tanzania dola milioni 800 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo

Picha
Marekani itatoa dola milioni 800 kwa Tanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress aliyekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo ni uthibitisho kuwa kutotolewa kwa fedha za awamu ya pili ya mradi wa changamoto za milenia (MCC-2) hakujaondoa uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Marekani ikiwemo utoaji wa misaada ya maendeleo. "Tumezungumza mambo kadhaa, na wiki hii Tanzania na Marekani kupitia shirika letu la misaada la USAID tunatarajia kutiliana saini mkataba wa zaidi ya dola milioni 400 kwa ajili ya mwaka ujao, pia tumezungumza kuwa kutakuwa na dola milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi mbalimbali na hii haihusiani na MCC. "Ukweli ni kwamba tunayo mengi ya kufanya pamoja katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu na kilimo na tutafanya kila juhudi kuhakikisha haya yanafanikiwa"  A...