Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wassira Amvaa January Makamba...... Asema Huenda Yeye ndo Alibebwa Tano Bora ya Urais CCM

Wassira Amvaa January Makamba...... Asema Huenda Yeye ndo Alibebwa Tano Bora ya Urais CCM

Picha
  MWANASIASA mkongwe aliyekuwa waziri katika Serikali ya awamu nne, Stephen Wasira, amemshangaa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba aliposema kuwa uwajibikaji katika utawala wa awamu ya nne ulikuwa ni wa kuleana. Kauli ya Wasira imekuja siku moja baada ya gazeti la Mwananchi kumnukuu Makamba akisema uwajibikaji katika Serikali ya awamu hiyo haukuwa wa kuridhisha kwasababu kulikuwa na utamaduni wa kuoneana haya, kujuana na kusitiriana. Akizungumza  katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam jana, Wasira alieleza kushangazwa na kauli hiyo ya Makamba akisema yawezekana aliyelelewa ni yeye. “Labda alilelewa yeye…kama rafiki yangu Makamba anasema kulikuwa na kuleana, mimi kwa upande wangu sikulelewa nilifanya kazi na nikatimiza wajibu wangu kama nilivyopewa na Rais. “Sasa kama aliona kulikuwa kuna kuleana mimi sijui yeye ndiye anajua maana mimi sikulelewa. Kama unafanya makosa halafu unaachwa huondolewi hapo ni kulean...