Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Atumbua Watumishi Watano Ilemela Kwa Tuhuma za ubadhirifu wa Fedha za Umma

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Atumbua Watumishi Watano Ilemela Kwa Tuhuma za ubadhirifu wa Fedha za Umma

Picha
Mkuu wa wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewasimamisha kazi maofisa watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka. Akiwa katika ziara ya siku moja ya kujitambulisha wilayani Ilemela leo, Mongella ameagiza kushushwa cheo kwa ofisa wa ardhi wa wilaya hiyo, Anicet Rweyemamu kwa tuhuma za kushindwa kusimamia watumishi walio chini yake wanaotuhumiwa kupokea Sh12 milioni kutoka kwa mwananchi mmoja aliyekuwa akitaka ardhi, lakini hajapewa hati hadi sasa. Wengine walioangukiwa na rungu la mkuu huyo ni Debora Tongora ambaye pamoja na Alex Chigulu wanatuhumiwa kupokea fedha hizo kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kuwapatia viwanja. Wakati Tongola tayari amefunguliwa mashtaka dhidi ya tuhuma hizo, Chigulu amehamishiwa mkoani Singida lakini Mongella ameagiza arejeshwe Mwanza ili afikishwe mahakamani. “RPC wasiliana na mwenzako wa Singida ili huyo mtumishi atiwe mbaroni muda huu na kesho arejeshwe Mwanza kukabiliana na ...