Mwigulu Nchemba Aapishwa Rasmi Kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.......Atoa ONYO Kali kwa Wauza Dawa za Kulevya
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo badala yake watafute shughuli halali za kujiingizia kipato. Waziri Nchemba ametoa agizo hilo mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyemteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mh.Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Aidha Waziri Nchemba alisema kuwa atahakikisha anasimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kwa kuziba mianya inayohatarisha amani na utulivu katika nchi. Naye Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa atahakikisha anashirikiana na wataalum wa sekta tatu zilizo katika Wizara yake ili kufanya mapinduzi katika maeneo hayo yaliyoajiri zaidi ya asiimia 80 ya Watanzania. Pia Waziri Dkt. Tizeba alisema kuwa Wizara itahakikisha inashugahulikia changamoto zinazozokabili v...