Samatta: Uwanja mzima SamaGoal
Kama ilivyo kwa Nigeria kupenda ligi mbalimbali duniani hasa Ligi Kuu ya England, lakini ndivyo ilivyo kwa Ghana na mataifa mengine ya Magharibi mwa Afrika. Pamoja na Watanzania wengi kupenda ligi hizo kwa mapenzi, mashabiki wa mataifa hayo hupenda ligi kubwa duniani kutokana na wachezaji wao kutawanyika huko. Huwezi kuwakosa raia wa Afrika Magharibi hasa Wanigeria katika ligi zote tano kubwa, EPL (England), Seria A (Italia), Lique 1 (Ufaransa), Bundesliga (Ujerumani) na La Liga ya Hispania. Watanzania wameanza kufuatilia na kuwa na mapenzi na Ligi ya Ubelgiji, Pro League na zaidi ni kuona mchezaji wao kipenzi, Mbwana Samatta, ‘SamaGoal’ akicheza huko katika klabu ya KRC Gent. Mpaka sasa, Samatta amecheza mechi nne, amefunga moja na ana kadi moja ya njano. Mechi mbili ambazo alitarajia kucheza ni dhidi ya Standard Liege, moja ya klabu zilizotisha Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akizungumza katika mahojiano na redio moja jijini Dar es Salaam, Samatta anasema: “Nilifurahi ...