MWANADADA AIKA ASEMA HAHITAJI KULIPIWA MAHARI NA NAHREEL
Aika na mpenzi wake, Nahreel. Wiki hii tunaye mwanadada anayeunda Kundi la Navy Kenzo anayefahamika kwa jina la Aika Mariale. Huyu ni mpenzi wa mwanamuziki na prodyuza aitwaye Nahreel. Amefunguka mambo mengi kuhusu usanii na maisha yake ya kimapenzi. Ungana na Mwandishi Wetu Hamida Hassan aliyembana kwa maswali 10. Ijumaa: Kwa nini uliamua kumkabidhi moyo wako Nahreel na si mwanaume mwingine? Aika: Ni mapenzi yangu kwake tu, si unajua tena kipenda roho! Ijumaa: Wewe na mpenzi wako mmedumu kwa muda mrefu, vipi suala la ndoa na mtoto? Aika: Ishu ya ndoa bado hatujapanga ila hilo la mtoto naamini tutampata Mungu akipenda. Ijumaa: Je, Nahreel akikutamkia ndoa utataka akulipie mahari ya shilingi ngapi? Aika: Mimi mahari sitaki, kwetu hamna utaratibu huo. Ijumaa: Ina maana utaolewa bure? Au ndiyo mambo ya huruma tena? Aika: Hapana, huo ni utaratibu wa familia yetu. Mambo ya mahari huwa hatuna. Ijumaa: Wewe ni msanii...