Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Familia Yasema Kifo cha Wilson Kabwe Hakikutokana na Mshtuko wa Kufukuzwa Kazi na Rais Magufuli

Familia Yasema Kifo cha Wilson Kabwe Hakikutokana na Mshtuko wa Kufukuzwa Kazi na Rais Magufuli

Picha
Familia ya Wilson Kabwe, aliyekuwa mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, imesema ndugu yao alishawatoa wasiwasi kuhusu tuhuma zilizosababisha kusimamishwa kazi na Rais John Magufuli na kwamba alitamani uchunguzi ufanyike haraka ili ukweli ujulikane.  Kabwe aliyefariki dunia Mei 20 kwa ugonjwa wa saratani ya tezi dume jijini Dar es Salaam, alisimamishwa kazi na Rais Magufuli wakati wa uzinduzi wa daraja la Mwalimu Nyerere lililopo Kigamboni Aprili 19.  Miongoni mwa makosa yaliyosababisha kusimamishwa kwake ni madai ya kusaini mkataba kwa kutumia sheria ndogo ya mwaka 2004 kutoza magari yanayotoka kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo (UBT) Sh4000 na mwingine wa Sh8,000 chini ya sheria ndogo mwaka 2009.  Kulikuwa pia na madai ya kukithiri kwa rushwa katika kituo hicho hasa katika kutoa magari na ukodishwaji wa vyumba vya kupangisha, kinyume na utaratibu na kuongeza muda wa mzabuni aliyeingia mkataba na jiji wa maegesho ya magari.  Akizungumza jana nyumbani kwao, Masak...